PRESS RELEASE
MSANII Joush Tasia Rhumba ambaye ni mahiri katika kucheza miondoko ya Salsa anatarajiwa kutoa burudani katika hafla ya uchangiaji wa fedha iliyoandaliwa na mfuko wa hisani ‘Blast From The Past Shear Charity Ball 2010’ iliyopangwa kufanyika Oktoba 2 katika hoteli ya Hilton iliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi katika hafla hiyo maalum atakuwa Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Januari Makamba .
Mbali ya uchangiaji fedha tukio kubwa ambalo ndilo limebeba hafla hii ni uzinduzi wa Jarida la ‘Shear Hair and Beauty Magazine’ ambalo liko sokoni kwa mwaka mmoja sasa linalozungumzia kuhusu mitindo ya nywele na vipodozi kwa wanawake kwa ambalo limepokelewa vizuri kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja na wateja wake wa kuaminika zaidi ya 5,000, ndani ya jarida hilo kuna masuala ya urembo na matunzo ya nywele sasa litazinduliwa rasmi nchini.
Kwa karne nyingi sasa masuala ya fasheni yametawala ubunifu wa mitindo yetu, hali ya jamii na utaalam. Tamasha la hisani la Shear linaloitwa kwa kimondo ‘Blast from the Past Shear Charity Ball’ au ‘Mlipuko toka Zamani’ litabeba ushuhuda wa mitindo mbalimbali na kuzindua rasmi jarida hili kwa soko lake la kuaminika, ambalo limeweza kulikuza.
Tamasha la ‘Blast from the Past’ litafanyika Hilton Hotel tarehe 2 Oktoba mwaka huu ambayo itakuwa ni maadhimisho rasmi ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya jarida lenyewe tangu lilipotoka kwa mara ya kwanza. Jarida hili limebeba hadhi na mwamko wa kimitindo kwa wabunifu maarufu wa mitindo nchini kutoka kwenye kada rasmi na watu wa kawaida. Tamasha hili la hisani litakuwa likifanyika kila mwaka kutambua mchango wa kuaminika wa wateja wa jarida hili na kuwahamasisha wateja wapya kuhusu kujiunga na familia ya Shear.
Mapato yatakayopatikana katika tukio hilo la hisani yataelekezwa kwenye mfuko wa taasisi ya CCBRT ambao hutunisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye ulemavu, ukijikita zaidi kwenye tatizo la Fistula, ambalo wanawake wanaosumbuliwa nalo hufanyiwa upasuaji bure katika hospitali ya taasisi hiyo.
Sehemu nyingine ya mapato hayo yatakwenda kwa ‘SOS Children’s Village’, kusaidia maisha ya watoto yatima na waliotelekezwa ambao husaidiwa na kituo hicho kinacholea watoto wakiwa katika makazi maalum yaliyo kama kijiji. Ujumbe wa tamasha hilo la hisani ni ‘60s, 70s’ na 80s’ ambapo wageni wote wanawake wataombwa kuvaa magauni mazuri ya tamasha hilo.
Mwisho
WAKO MTIFU,
_____________________
SUZAN MISEDA
MSEMAJI, SHEAR CHARITY BALL